Mchanganuo wa sababu zinazofanya mtu kuendelea kuwa na kitambi:
1. Unaanza kuzeeka
Kadiri unavyozeeka, mwili wako unabadili jinsi unavyo
ongezeka na kupunguza uzito. Jinsi zote; za kike na kiume, hupatwa na kupungua
kwa utendaji wa kimetaboliki, kutia ndani kiasi cha kalori zinazohitajika kwa
mwili kufanya kazi kwa ukawaida.
Zaidi ya hayo wanawake hupatwa na kukoma kwa hedhi, ikiwa
wanawake wataongezeka uzito, mara nyingi uzito huo huwa kwenye matumbo yao.
Wakati wa kukoma kwa hedhi, uzalishaji wa homoni za
Istrojeni na Projesteroni hupungua. Wakati huo huo homoni ya testosteroni
huanza kupungua kidogo kidogo. Mabadiliko ya homoni hufanya wanawake wengi
kuendelea kubeba uzito mwingi kwenye matumbo yao.
2. Kutofanya mazoezi kwa usahihi.
Mazoezi ya kulala chali na kuinua mwili kuanzia kiuno hadi
kichwa (Crunches)
sio mazoezi yatakayokusaidia kuondoa kitambi. Badala yake
fanya mazoezi ya stamina yatakayo kufanya utumie nyama (muscles) za tumbo,
mgongo, nyonga na sehemu zingine za mwili. Kufanya mazoezi ya namna hii
kutasaidia kuunguza/kutumia kalori nyingi mwilini na hivyo kufanya mafuta
yaliyo maeneo ya tumbo kutumika pia.
Mazoezi ya kukaa kwa muda jinsi fulani kama unapiga pushapu
kitaalamu hujulikana kama Plunk(picha hapo chini), ndio mazoezi yanayofaa kwa
kuwa huhusisha matumizi ya nyama za mikono, miguu na makalio.
Kukimbia kila siku ni mazoezi bora kwa mwili na moyo wako
ingawa mazoezi kwa ajili ya moyo wenye afya peke yake hayawezi kusaidia maeneo
ya kiunoni kutia ndani kitambi.
“kitaalamu inapendekezwa dakika 250 za mazoezi ya kawaida au
dakika 125 za mazoezi magumu kila wiki.
3. Una mkazo
Kuwa na majukumu mengi ya kikazi, familia, kulipa gharama za
shule na bili mbalimbali kama umeme na maji kunaweza kufanya ugumu katika
kupunguza uzito usiotakiwa mwilini, hasa kuanzia umri wa kati. Homoni ya mkazo
iitwayo Cortisol huongeza kiwango cha mafuta kinachochukuliwa mwilini na
kutanua seli za mafuta. Uwepo wa kiwango kikubwa cha homoni hii huhusiana kwa
karibu na ongezeko la mafuta mwilini.
4. Unajinyima usingizi wa kutosha.
Kama wewe ni mmoja ya watu wale wanaokosa muda wa kutosha
kulala kwa ajili ya mihangaiko ya hapa na pale unapaswa kuongeza muda wako wa
kupumzika. Utafiti uliofanywa kwa miaka 16 kwa wanawake 70,000 ulibaini
wanawake waliolala masaa matano au chini ya hapo walitarajiwa kuongezeka kilo
14 kuliko wale waliolala masaa 7. Wataalamu hushauri watu wazima kulala masaa 7
hadi 8 wakati wa usiku.
5. Una maradhi.
Ikiwa kiwango chako cha homoni ya testosteroni kiko juu
inaweza kuashiria kutokea kwa ugonjwa wa ovari (PCOS) ugonjwa utakaosababisha
iwe vigumu kupunguza uzito. “Ikiwa una umbo la tufaa na una uzito uliozidi
kiasi, ni busara kumuona daktari” kwa maana hali hiyo inaongeza hatari ya
kupatwa na ugonjwa wa kisukari.
6. Mazoezi unayofanya hayatii
changamoto za kutosha katika mwili.
Ili kuondoa kitambi cha muda mrefu ni lazima kujidhatiti
kwenye mazoezi magumu. Utafiti uliochapishwa na Jarida Medicine and Science in
Sports and Exercises, ulionyesha watu waliofanya mazoezi magumu/mazito waliweza
kupunguza kitambi haraka zaidi kuliko waliofanya mazoezi mepesi. “Ikiwa lengo
lako ni kuondoa kitambi kabisa, basi huna budi kuchagua mazoezi kuondoa
kitambi” asema Natalie Jill, mtaalamu wa mazoezi kutoka San Diego.
7. Unakula mafutayasiyohitajika
mwilini
Mwili haumeng’enyi aina zote za mafuta kwa njia ileile.
Utafiti unaonyesha ulaji wa vyakula vyenye mafuta kama nyama na maziwa huongeza
mafuta tumboni na hufanya kitambi. Wakati ulaji wa vyakula vya mafuta kama
parachichi, samaki na alizeti huuweka mwili katika umbo zuri. Ingawa kula
vyakula vyenye mafuta ya aina yoyote hufanya mwili kuongeza uzito na
kusababisha kitambi hivyo ni vizuri kufurahia vyakula hivyo kwa kiasi.
8. Unakula sana vyakula
vilivyosindikwa viwandani.
Vyakula kama mkate mweupe, chipsi, vinywaji vyenye sukari
kama soda, juisi hufanya mwili kutanuka/kunenepa. Kitambi huambatana na
kunenepa/kutanuka kwa mwili, hivyo ulaji wa vyakula vya viwandani utarudisha
nyuma jitihada/uwezo wako wa kupambana na kitambi. Vyakula vya asili kama
matunda, mbogamboga na nafaka isiyokobolewa ambavyo ni vya asili huufanya mwili
kusinyaa na kusaidia kuzuia kitambi.
9. Hauna hamasa (motisha).
Ni kweli uko tayari kisawasawa kuondoa kitambi? “Kupunguza
na kuondoa kitambi kunahitaji ushirikiano wa vitu mbalimbali, vyakula vyenye
kutia nguvu kidogo na vyenye nyuzinyuzi kwa wingi pamoja na vyakula vyenye
wanga na sukari kidogo huku ukifanya mazoezi ya kupunguza uzito.” Dk Kashyap
anasema. Ikiwa umepania kupunguza/kuondoa kitambi unaweza kufanikiwa.
(10) Una umbo la tufaha (apple)
“Ikiwa unene wako upo maeneo ya katikati tofauti na maeneo
ya hipsi (nyonga) na mapaja basi una umbo la tufaha (apple). Kwa muundo huu wa
mwili ikiwa ni wa kurithi basi kupunguza kitambi, itakuwa ngumu sana,” anasema
Dk Kashyap.
No comments:
Post a Comment