Thursday, 15 November 2018







UFAFANUZI KUHUSU MAANA YA MICHORO YA BARABARANI*
. *MICHORO YA BARABARANI*
Michoro ya barabarani pia imegawanyika katika mafungu makuu matatu
(a) Michoro ya udhibiti (regulatory)
Ni lazima kutii michoro hii kwani ukiukwaji wake ni kosa linalopelekea adhabu. Michoro ya kundi la udhibiti ni pamoja na:
1. STOP LINE-Huu ni mstari au mraba mweupe unaokuwepo kwenye makutano ya barabara
2. TOA NJIA-huu ni stari unaokuwepo barabarani hasa kwenye makutano ukiwa na mkato mkato ukimuamuru dereva kutoa njia
3. Michoro ya Zebra
4. USIOVATEKI-Mstari mmoja mweupe usiokatika katika katikati ya barabara
5. USIVUKE MSTARI-Hii nbi mistari miwili au mirtaba miwili myeupe katikati ya barabara. Nayo tumezoea kuiita MARUFUKU KUOVATEKI.
6. MSTARI WA UKINGO (Edege line)-huu ni mstari wa njano pembeni mwa barabara
7. MSTARI WA ZIGZAGA
8. NA MINGINEYO
(b) Michoro ya tahadhari (warning)
Hii ni kama ilivyoelezwa hapo juu kwenye alama za onyo.
(c) Michoro ya mwongozo (guidance)
Kwa mujibu wa muongozo wa TANROADS wa usimikaji alama na uchoraji wa michoro, maneno yaliyochora chini yanayosema STOP(GM7) ni alama ya mwongozo/maelekezo ikiwa rangi iliyotumika kuchora ni NYEUPE. Pia neno 5O likichorwa kwenye duara nyeupe na hamisni yenyewe kuwa nyeupe basi hiyo inaingia kwenye maelekezo. Mchoro huo unakuongoza kupunguza mwendo. Hivyo mtu hapaswi kuadhibiwa kwa kukiuka alama ya tahadhari au ya muongozo/maelekezo.
Ni matumaini yangu kwa maelezo haya umeongeza maarifa kuhusu usalama barabarani.
RSAadmin1
RSA TANZANIA
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.

No comments:

Post a Comment

MATOKEO YA AWALI ENTERPRENEURSHIP LEVEL 6-2. KUNA AMBAO KATI ONE ITARUDI ILE YA MWANZO.

TABORA POLYTECHNIC COLLEGE PHARMACEUTICAL SCIENCES DEPARTMENT EXAMINATION NUMBER  NTA LEVEL 6...