Saturday, 5 October 2019

MFAHAMU KANGAROO !MUNGU KWELI KAUMBA VINGI VYA KUSHANGAZA
"Kangaroo ni mnyama mwenye ufanano wa sura kwa mbali na sungura, wanyama hawa huwa na miguu mifupi sana ya mbele, kiasi cha kumfanya hata akimbiapo kutumia miguu miwili ya nyuma huku mkia wake ukimpa msaada mkubwa katika balance ya mwili, pamoja kwamba hukimbia kwa kunesa kama spring, lakini wakati mwingine mnyama huyu hutumia pia miguu yake ya mbele kutembelea hasa anapokula na kucheza na mtoto wake.""
""Madume wa kangaroo huwa wakubwa kuliko majike, wanyama hawa hufikia uzito wa kilo mpaka 90 na urefu wa futi sita, pia dume hutofautiana na jike kwa kwa muonekano wa rangi ambapo dume huwa kama wekundu kidogo mgongoni na majike huwa wakijivu.""
"Mnyama huyu ni miongoni mwa wanyama wanaokimbia sana, lakini kwa kuwa hutumia miguu miwili bahati yake huwa mbaya anapowindwa na wanyama walao nyama kama simba, kwakuwa hukosa uwezo wa kushindana nao mbio.""
""Kangaroo ni mnyama mpenda amani na si mkorofi hata kwa mtoto wake, isipokuwa madume tuu ndio hupigana hasa wanapopenda sehemu moja, na mapigano yao ni ya kustaajabisha miguu ya mbele hutumia kwa kushikana huku wakitumia miguu yao kupigania na hurusha mateke yake kwa miguu yote, huku mkia wake mrefu ukimpa sapoti ya kuweka sawa mwili wake.""
""Wanyama hawa hutumia pua zao vyema kunusa, na huwatambua maadui kwa kunusa tuu, maadui wake wakubwa ni wawili yaani simba pamoja na ndege tai, ambaye mara kwa mara hufanya majaribio ya kutaka kuiba watoto wa kangaroo.""
""Kangaroo jike ana mfuko ambao hutumia kubebea mtoto wake, mara zote ahisipo hatari humuingiza mtoto wake katika mfuko huo, na kisha kutoweka maeneo hayo na hata mtoto pia hujihami kwa kuingia katika mfuko wa mama aonapo kuna tatizo.""
""Jike limvutia dume kwa ajili ya mahaba, dume hunusa kwanza mkojo wake kutambua kama jike huyo yu salama au anataka kumuuzia kesi ya Mimba, hata hivyo jambo la kustaajabisha ni kwamba kangaroo endapo atapata mimba wakati mtoto wake bado ananyonya huweza kuzuia mimba hiyo isikue mpaka hapo atakapo muondoa mtoto aliyenaye kwa wakati huo.""
""Kama sisi tunavyomuheshimu twiga ndivyo hivyo hivyo anavyoheshimika kangaroo nchini Australia, Ni alama ya utambulisho wa taifa lao, pia amewekwa katika ngao ya taifa lao pia, ni mnyama anayependwa sana nchini humo.""
""Kwa bahati mbaya Tanzania hakuna kangaroo kabisa, lakini cha kufahamu ni kwamba wanyama hawa hupendelea kuishi maeneo kame, na chakula chao kikuu ni majani tuu, alapo majani chakula kingine huweka akiba tumboni mwake, hivyo muda apumzikao hucheua na kuanza kula upyaa kama wafanyavyo mbuzi au ng'ombe.""
Sifa zake.
 Ana uwezo wa kukimbia km 22 kwa saa moja.
 Kuogelea kwake sio ishu na akimbiapo anaweza katisha katika maji.
 Wakati wa jua Kali hupumzika, jioni asubuhi ndio mida ambayo hupendelea kula.
 Ana uwezo wa kuzuia mimba yake isikue.
 huishi katika makundi yanayozidi kangaroo kumi.
 kusalimiana kwa kangaroo ni kitu cha kawaida kama ilivyo kwetu.
 Ujanja wote kangaroo hawezi kutembea kinyume nyume.
 katika mfuko wake anaweza kuwaingiza hata watoto wawili.
 Ukimshitua au ikitokea hatari anaweza kuruka zaidi ya foot kumi na tano, kwahiyo hizo fensi za nyumba kwa kangaroo sio ishu kuruka pasina kugusa ukuta.
 Akili zake huamini kua Yeye na Binadamu Hufanana.

ZIFAHAMU SHERIA ZAKO ZA MSINGI UKIKUTANA POLISI USINYANYASWE FANYA HAYA UWAPO MIKONONI MWA POLISI

IMEANDALIWA NA MAWAKILI
  • 1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.

  • 2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
  • 4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
  • 5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
  • 6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.
  • 7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
  • 8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
  • 9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
  • 10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
  • 11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
  • 12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.
  • 13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
  • 14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.
  • 15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.
  • 16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.
  • 17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
  • 18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
  • 19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.
  • 20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
  • 21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.
  • 22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
  • SHARE KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ILI WAZIFAHAMU HAKI ZAO

MATOKEO YA AWALI ENTERPRENEURSHIP LEVEL 6-2. KUNA AMBAO KATI ONE ITARUDI ILE YA MWANZO.

TABORA POLYTECHNIC COLLEGE PHARMACEUTICAL SCIENCES DEPARTMENT EXAMINATION NUMBER  NTA LEVEL 6...