Saturday, 5 October 2019

MFAHAMU KANGAROO !MUNGU KWELI KAUMBA VINGI VYA KUSHANGAZA
"Kangaroo ni mnyama mwenye ufanano wa sura kwa mbali na sungura, wanyama hawa huwa na miguu mifupi sana ya mbele, kiasi cha kumfanya hata akimbiapo kutumia miguu miwili ya nyuma huku mkia wake ukimpa msaada mkubwa katika balance ya mwili, pamoja kwamba hukimbia kwa kunesa kama spring, lakini wakati mwingine mnyama huyu hutumia pia miguu yake ya mbele kutembelea hasa anapokula na kucheza na mtoto wake.""
""Madume wa kangaroo huwa wakubwa kuliko majike, wanyama hawa hufikia uzito wa kilo mpaka 90 na urefu wa futi sita, pia dume hutofautiana na jike kwa kwa muonekano wa rangi ambapo dume huwa kama wekundu kidogo mgongoni na majike huwa wakijivu.""
"Mnyama huyu ni miongoni mwa wanyama wanaokimbia sana, lakini kwa kuwa hutumia miguu miwili bahati yake huwa mbaya anapowindwa na wanyama walao nyama kama simba, kwakuwa hukosa uwezo wa kushindana nao mbio.""
""Kangaroo ni mnyama mpenda amani na si mkorofi hata kwa mtoto wake, isipokuwa madume tuu ndio hupigana hasa wanapopenda sehemu moja, na mapigano yao ni ya kustaajabisha miguu ya mbele hutumia kwa kushikana huku wakitumia miguu yao kupigania na hurusha mateke yake kwa miguu yote, huku mkia wake mrefu ukimpa sapoti ya kuweka sawa mwili wake.""
""Wanyama hawa hutumia pua zao vyema kunusa, na huwatambua maadui kwa kunusa tuu, maadui wake wakubwa ni wawili yaani simba pamoja na ndege tai, ambaye mara kwa mara hufanya majaribio ya kutaka kuiba watoto wa kangaroo.""
""Kangaroo jike ana mfuko ambao hutumia kubebea mtoto wake, mara zote ahisipo hatari humuingiza mtoto wake katika mfuko huo, na kisha kutoweka maeneo hayo na hata mtoto pia hujihami kwa kuingia katika mfuko wa mama aonapo kuna tatizo.""
""Jike limvutia dume kwa ajili ya mahaba, dume hunusa kwanza mkojo wake kutambua kama jike huyo yu salama au anataka kumuuzia kesi ya Mimba, hata hivyo jambo la kustaajabisha ni kwamba kangaroo endapo atapata mimba wakati mtoto wake bado ananyonya huweza kuzuia mimba hiyo isikue mpaka hapo atakapo muondoa mtoto aliyenaye kwa wakati huo.""
""Kama sisi tunavyomuheshimu twiga ndivyo hivyo hivyo anavyoheshimika kangaroo nchini Australia, Ni alama ya utambulisho wa taifa lao, pia amewekwa katika ngao ya taifa lao pia, ni mnyama anayependwa sana nchini humo.""
""Kwa bahati mbaya Tanzania hakuna kangaroo kabisa, lakini cha kufahamu ni kwamba wanyama hawa hupendelea kuishi maeneo kame, na chakula chao kikuu ni majani tuu, alapo majani chakula kingine huweka akiba tumboni mwake, hivyo muda apumzikao hucheua na kuanza kula upyaa kama wafanyavyo mbuzi au ng'ombe.""
Sifa zake.
 Ana uwezo wa kukimbia km 22 kwa saa moja.
 Kuogelea kwake sio ishu na akimbiapo anaweza katisha katika maji.
 Wakati wa jua Kali hupumzika, jioni asubuhi ndio mida ambayo hupendelea kula.
 Ana uwezo wa kuzuia mimba yake isikue.
 huishi katika makundi yanayozidi kangaroo kumi.
 kusalimiana kwa kangaroo ni kitu cha kawaida kama ilivyo kwetu.
 Ujanja wote kangaroo hawezi kutembea kinyume nyume.
 katika mfuko wake anaweza kuwaingiza hata watoto wawili.
 Ukimshitua au ikitokea hatari anaweza kuruka zaidi ya foot kumi na tano, kwahiyo hizo fensi za nyumba kwa kangaroo sio ishu kuruka pasina kugusa ukuta.
 Akili zake huamini kua Yeye na Binadamu Hufanana.

4 comments:

  1. Bet365 casino bonus codes | DrMCD
    What 경산 출장안마 is bet365 casino? All bet365 밀양 출장마사지 bonus codes 청주 출장샵 must be claimed on your 익산 출장마사지 first deposit of at least £10, not more than 8 경산 출장샵 times in your casino account.

    ReplyDelete

MATOKEO YA AWALI ENTERPRENEURSHIP LEVEL 6-2. KUNA AMBAO KATI ONE ITARUDI ILE YA MWANZO.

TABORA POLYTECHNIC COLLEGE PHARMACEUTICAL SCIENCES DEPARTMENT EXAMINATION NUMBER  NTA LEVEL 6...