ZIFAHAMU SHERIA ZAKO ZA MSINGI UKIKUTANA POLISI USINYANYASWE FANYA HAYA UWAPO MIKONONI MWA POLISI
IMEANDALIWA NA MAWAKILI
- 1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.
- 2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
- 4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
- 5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
- 6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.
- 7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
- 8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
- 9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
- 10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
- 11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
- 12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.
- 13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
- 14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.
- 15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.
- 16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.
- 17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
- 18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
- 19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.
- 20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
- 21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.
- 22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
- SHARE KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ILI WAZIFAHAMU HAKI ZAO
No comments:
Post a Comment